Vinjari kwa Herufi

Herufi: M

Vimepatikana vidahizo 3,098 vinavyoanza na herufi M.

Ukurasa 48 / 62 Jumla 3,098

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

msunguti

1. Mti wenye shina la majimaji unaohusishwa na sumu ya mishale ya uwindaji. 2. Yenye ladha kali.

msusu

1. Mti wenye mizizi inayotumiwa katika tiba za jadi za magonjwa ya zinaa. 2. Mkia wa kuku au ndege mwingine.

msuuzo

1. Mkono au kifaa cha kulishikia jiwe la kusagia. 2. Maji safi ya mwisho ya kuondoa sabuni au uchafu kwenye kitu kilichooshwa. 3. Tendo la kupiti...

Mswahili

1. Mwenyeji wa pwani ya Afrika Mashariki ambaye Kiswahili ni lugha yake ya kwanza. 2. Mkazi wa mjini anayezungumza Kiswahili kama lugha ya kwanza....

mswaki

1. Kijiti kibichi au brashi yenye mpini ya kusafishia meno. 2. Mti wa kijivu wenye vitawi vinavyotumiwa kusugulia meno.

mswano

1. Ladha tamu ya kitu kinacholiwa, hasa muwa. 2. Hali ya kutengemaa na kuwa katika utulivu.

mtaa

1. Eneo kubwa kuliko kitongoji lililojitenga na mji. 2. Barabara ya mjini pamoja na eneo linaloizunguka.

mtaguso

Mkutano maalumu wa viongozi wa Kanisa Katoliki wa kujadili na kuamua masuala ya Kanisa.

mtai

1. Alama iliyochanjwa au kukwaruzwa mwilini. 2. Mstari unaopita kwa mshazari.

mtaji

1. Fedha au mali ya kuanzishia au kukuza biashara. 2. Chungu ya komwe inayowezesha kula kete za mpinzani katika bao.

mtakato

1. Hali ya kushindwa kula kete za bao kwa kukosa mtaji. 2. Usafi wa mtu, hasa katika mavazi.