Vinjari kwa Herufi

Herufi: M

Vimepatikana vidahizo 3,098 vinavyoanza na herufi M.

Ukurasa 50 / 62 Jumla 3,098

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

mtawa

1. Mcha Mungu anayeishi katika makazi maalumu mbali na maisha ya watu wengi. 2. Mwanamke anayewekwa nyumbani ili asitoke bila mipaka.

mtegaji

1. Mtu anayejiepusha na kufanya kazi. 2. Mtu anayeweka kifaa cha kunasia wanyama au samaki.

mtegeaji

1. Mtu anayeandaa mtego wa kukamata kitu, hasa samaki. 2. Mtu anayekwepa kazi kwa visingizio lakini anataka malipo yake.

mtego

1. Kifaa cha kukamatia mnyama, ndege au samaki. 2. Tendo la kutayarisha hali au kifaa cha kunasia. 3. Mbinu anayotumia mtu ili kupata anachokitaka.

mteguko

1. Hali ya kitu kutoka katika nafasi yake ya kawaida. 2. Katika fasihi, tukio jipya kushika kasi hadi la awali lisahaulike.

mteja

1. Mtu anayenunua bidhaa au kutumia huduma za mahali fulani. 2. Mtu anayekwenda kwa mganga wa jadi kwa ramli au tiba.

mtembezi

1. Mtu anayependa kwenda huku na huku bila kutulia. 2. Mtu mwenye hamu kubwa ya kujihusisha na ngono.

mtembo

1. Mipasuko inayotokea kwenye visigino vya miguu. 2. Moyo laini unaopatikana kileleni mwa mnazi.

mtemi

1. Kiongozi wa kimila wa kabila, hasa katika jamii za Tanzania. 2. Mtu mwenye nguvu anayeweza kuwapiga wengine.

mtenzi

1. Mtunzi wa mashairi, tenzi au nyimbo. 2. Mtu mwenye uwezo wa kutekeleza jambo.

mtesi

1. Mtu mwenye mazoea ya kuwasema wengine vibaya. 2. Mtu anayependa kugombana.