Vinjari kwa Silabi

Silabi: sha

Vimepatikana vidahizo 356 vinavyoishia kwa silabi sha.

Ukurasa 6 / 8 Jumla 356

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

sasisha

1. Badili mtindo wa zamani ulingane na wa sasa. 2. Rekebisha hali isiyoridhisha iwe nzuri zaidi.

shisha

1. Chombo cha kioo kinachotumiwa kupima kupita kwa muda. 2. Kifaa cha kuvutia tumbaku chenye bomba na chombo cha maji.

shusha

1. Teremsha kitu au mwache abiria atoke chomboni. 2. Toa shahawa wakati wa tendo la ngono.

simamisha

1. Fanya mtu au kitu kiinuke kiwe wima. 2. Zuia mwendo au shughuli isiendelee. 3. Mteue mtu awe mgombea wa nafasi ya uongozi. 4. Weka kitu kikae...

stusha

1. Sababisha taharuki kwa mtu au mnyama. 2. Fanya kiungo kisikae au kisifanye kazi sawasawa.

swahilisha

1. Rekebisha neno la kigeni lifuate sarufi ya Kiswahili. 2. Mfundishe mtu utamaduni na mwenendo wa Waswahili.

tapisha

1. Sababisha mtu atapike. 2. Ondoa kinyesi katika choo kilichojaa. 3. Mpe mwari mafunzo ya mwisho ya unyagoni.

teremsha

1. Hamisha kitu kutoka juu na kukileta chini. 2. Mwezeshe abiria kutoka katika chombo cha usafiri.