Vinjari kwa Silabi

Silabi: na

Vimepatikana vidahizo 310 vinavyoishia kwa silabi na.

Ukurasa 1 / 7 Jumla 310

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

achana

1. Kutengana na mtu uliyekuwa naye katika uhusiano, hasa mke au mume. 2. Kutengana kwa vitu vilivyokuwa vimeshikana, kila kimoja kikawa peke yake ...

agana

1. Kukubaliana na mtu mwingine kwamba mtafanya jambo fulani. 2. Kuambiana kwaheri na kutakiana heri wakati wa kuachana.

akina

Kundi la watu wanaotajwa pamoja kwa jina, uhusiano au sifa inayowaunganisha.

amana

1. Kitu anachokabidhiwa mtu na mwingine akitunze au akihifadhi kwa niaba yake. 2. Kitu au mali iliyohifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya baadaye; ak...

ambizana

1. Kupeana habari au kueleza jambo kwa zamu baina ya watu. 2. Kuelezana misimamo au maoni kuhusu jambo fulani.

antena

Kifaa cha kupokea au kutuma mawimbi ya redio yanayobeba taarifa kama sauti na picha.

antifona

1. Wimbo wa ibada unaoimbwa kabla ya kusoma au kuimba zaburi. 2. Wimbo wa Kikristo unaoimbwa wakati wa ibada.

babewana

Ndege wa jamii ya bundi mwenye macho makubwa ya duara, anayehusishwa na mikosi katika baadhi ya imani za jadi.

baina

Neno linaloonyesha kuwa jambo au kitu kiko kati ya watu au vitu viwili au zaidi.

bana

1. Kusonga kitu kwa nguvu kutoka pande mbili au zaidi; kugandamiza. 2. Kukamata na kushikilia kwa nguvu ili kitu kisitoroke. 3. Kufunga kitu vizu...

bayana

1. Ushahidi wa maneno au vitu unaotolewa kuthibitisha madai. 2. Kwa uwazi bila kuficha jambo.

bebena

1. Kukata kitu kidogokidogo kwa meno ya mbele. 2. Kukata chakula kwa meno ya mbele kisha kukitafuna kwa magego.

Bwana

1. Jina la heshima linalotumiwa kumtaja au kumwita mwanaume. 2. Mwanaume aliye katika ndoa; mume. 3. Mwanaume anayemwajiri mtu na kuwa na mamlaka...

chana

1. Pasua kitu kwa kukirarua au kukikata katika sehemu. 2. Pitisha kitana katika nywele ili kuzipanga au kuzifumua. 3. Muundo wa nta wenye vijumba...

china

1. Haribika kwa kukaa muda mrefu, hasa nyama au samaki waliowekwa mahali penye joto. 2. Shindwa kupata kitu au kutimiza jambo ulilotarajia. 3. Wa...

chukuana

1. Fuatana au andamana pamoja. 2. Lingana kwa tabia. 3. Faa kuwekwa au kuwa pamoja. 4. Elewana, pendana au faana.

chuna

1. Ondoa au bandua ngozi au ganda. 2. Kwaruza au chubua uso wa kitu. 3. Katika tungo za nahau, pata fedha kutoka kwa mtu kwa kumtumia au kumlaghai.

dafina

1. Hazina iliyofichwa chini ya ardhi. 2. Zawadi au kitu cha thamani kilichopatikana bila kutarajiwa.

danadana

1. Kwa juu juu bila kuzama katika jambo. 2. Kwa shangwe na vifijo. 3. Upigaji wa mpira kwa viungo mbalimbali bila kuuacha uguse chini. 4. Uzungu...

dhamana

1. Fedha au mali inayowekwa kuhakikisha utekelezaji wa wajibu. 2. Wajibu au mamlaka ya kushughulikia jambo kwa niaba ya wengine.

dona

1. Unga wa mahindi yaliyosagwa bila kukobolewa. 2. Okota kitu kimoja kimoja kwa mdomo, hasa kwa ndege.