Vinjari kwa Silabi

Silabi: ti

Vimepatikana vidahizo 299 vinavyoishia kwa silabi ti.

Ukurasa 4 / 6 Jumla 299

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

mlingoti

1. Shina refu la maua linalochomoza katika mkonge. 2. Nguzo iliyosimamishwa kwa ajili ya kupandisha bendera. 3. Nguzo ndefu ya chombo cha majini ...

msaliti

1. Mtu anayewapa maadui siri za nchi yake ili kuihujumu. 2. Mwanachama anayewapa wapinzani siri za chama au jumuiya yake.

msunguti

1. Mti wenye shina la majimaji unaohusishwa na sumu ya mishale ya uwindaji. 2. Yenye ladha kali.

njiti

1. Vijiti vya kiberiti vyenye kichwa cha kuwashia moto. 2. Mtoto aliyezaliwa kabla ya mimba kukamilisha muda wake wa kawaida.

noti

1. Karatasi maalumu inayotambuliwa rasmi kama pesa. 2. Alama ya maandishi inayowakilisha sauti ya muziki.

nyeti

1. Inayohitaji tahadhari kwa siri, masilahi au hisia zinazohusika. 2. Sehemu za siri za mwanamume au mwanamke.