Vinjari kwa Silabi

Silabi: ti

Vimepatikana vidahizo 299 vinavyoishia kwa silabi ti.

Ukurasa 3 / 6 Jumla 299

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

kati

1. Baina ya vitu au maeneo yanayotajwa. 2. Miongoni mwa kundi linalotajwa.

kibiriti

1. Kisanduku cha njiti za kuwashia moto au kifaa kidogo cha kuwashia. 2. Dawa inayotumiwa kutibu upele.

kiti

1. Samani iliyotengenezwa kwa kukaliwa. 2. Sehemu ya mbao ya chini ya paa ndani ya dau aina ya mtepe. 3. Mtu anayeaminika kuingiwa au kupagawa na...

kizingiti

1. Ubao wa juu au wa chini katika fremu ya mlango au dirisha. 2. Njia ya kuingilia majini kutoka ukingoni. 3. Jambo linalozuia mtu kutekeleza ali...

kombati

1. Mavazi yanayovaliwa na wanajeshi. 2. Fito za kufungia kiambaza kabla ya kukandika. 3. Miti mirefu myembamba inayotumiwa kujengea.

kreti

1. Sanduku la kuhifadhia na kubebea chupa za vinywaji. 2. Sanduku la mbao la kusafirishia bidhaa kama matunda.

kunuti

1. Dua inayosomwa katika swala ya alfajiri kwa utaratibu unaoifuata. 2. Omba dua kwa Mwenyezi Mungu.

lifti

1. Chombo cha umeme cha kusafirisha watu kati ya ghorofa. 2. Msaada wa kubebwa safarini bila kulipa nauli.

mahati

1. Kifaa cha seremala chenye ncha ya kuchora mstari. 2. Kamba inayotumiwa kuweka mstari wa mwongozo.