Vinjari kwa Silabi

Silabi: mu

Vimepatikana vidahizo 270 vinavyoishia kwa silabi mu.

Ukurasa 4 / 6 Jumla 270

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

mnajimu

1. Mtu anayetabiri matukio kwa kutafsiri nyota. 2. Mwenye maarifa ya mienendo ya nyota.

mzimu

1. Mahali pa tambiko panapoaminiwa kukaa roho za wazee waliofariki. 2. Pango au mti mkubwa unaoaminiwa kuwa makao ya pepo wa eneo. 3. Taswira ya ...

ngumu

1. Isiyo laini inapoguswa au kubanwa. 2. Isiyo rahisi kufanywa au kutimizwa. 3. Isiyoeleweka kwa urahisi.

nidhamu

1. Tabia nzuri inayozingatia maadili na heshima. 2. Utaratibu mzuri wa kuendesha shughuli.

njumu

1. Misumari inayowekwa kwenye soli za viatu vya michezo. 2. Misumari ya mapambo yenye vichwa vya shaba.

plamu

Tunda tamu lenye nyama nyingi na rangi ya zambarau, nyekundu au njano likiiva.

programu

1. Mpango unaoweka utaratibu wa kutekeleza jambo. 2. Mfuatano wa maagizo unaowezesha kompyuta kutekeleza kazi.

pumu

Ugonjwa wa njia za hewa unaoweza kusababisha kubanwa kifua na shida ya kupumua.

salamu

1. Maneno ya kumjulia mtu hali. 2. Ujumbe unaokabidhiwa mtu aupeleke kwa mwingine.

salimu

1. Mpelekee mtu maneno ya maamkizi na heri. 2. Kubali kuwa umeshindwa na uache upinzani.