Vinjari kwa Silabi

Silabi: li

Vimepatikana vidahizo 413 vinavyoishia kwa silabi li.

Ukurasa 3 / 9 Jumla 413

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

goli

1. Bao linalopatikana kwa kuingiza mpira mahali panapolengwa. 2. Eneo au kifaa kinacholengwa kuingiziwa mpira ili kupata bao.

gololi

1. Kitufe kidogo cha duara kinachotumiwa katika mchezo wa watoto. 2. Kokwa moja ya pumbu. 3. Utandu mweupe katika jicho unaoathiri kuona.

hali

1. Namna kitu au mambo yalivyo kwa wakati fulani. 2. Neno linaloonyesha hali halisi iliyo kinyume na kinachotajwa.

hoteli

1. Mahali pa kununua vyakula na vinywaji. 2. Jengo la kupangisha wageni vyumba vya kulala.

ingilia

1. Jitie katika mazungumzo bila kupewa nafasi. 2. Tenganisha wanaogombana ili kuzuia mapigano. 3. Fanya tendo la ngono na mtu.

jabali

1. Jiwe kubwa sana linalochomoza ardhini. 2. Mlima wa mwamba au miamba iliyo wazi. 3. Mshono wa nyuma ya kanzu kati ya mabega.

jahili

1. Mtu mwenye ugumu mkubwa wa kuelewa. 2. Mtu asiye na ujuzi wa jambo fulani. 3. Mtu mwenye ukatili mkubwa.

jali

1. Tilia jambo maanani na kulifanya ipasavyo. 2. Thamini mtu na kumhudumia kwa heshima.

kabali

1. Mshiko wa shingo unaozuia mtu kufurukuta. 2. Ukabaji wa mtu shingoni kwa nia ya kumdhuru.

kabili

1. Simama mbele ya mwingine tayari kupambana. 2. Elekea upande wa mbele wa kitu. 3. Mtu mwenye ujuzi wa kupiga zumari. 4. Mwenye ushujaa au uimara.

kali

1. Yenye uwezo wa kukata au kuchoma kwa ncha. 2. Yenye tabia ya kuumiza au kukaripia. 3. Yenye ladha inayowasha kama pilipili. 4. Yenye nguvu ku...