Vinjari kwa Herufi

Herufi: P

Vimepatikana vidahizo 574 vinavyoanza na herufi P.

Ukurasa 10 / 12 Jumla 574

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

potea

1. Kuwa mahali pasipojulikana au kutoweza kuonekana. 2. Badilika kutoka tabia nzuri na kuingia katika mienendo mibaya. 3. Kosa njia sahihi ya kuf...

poteza

1. Fanya kitu kisipatikane au kisionekane kilipo. 2. Tumia kitu bila manufaa au kwa uzembe.

potoa

1. Mfundishe au mwelekeze mtu katika tabia mbaya. 2. Badili maana ya jambo hadi isipatikane kama ilivyokusudiwa. 3. Vuruga au chafua kitu kilicho...

potoka

1. Fuata mwenendo au tabia inayochukuliwa kuwa mbaya. 2. Haribika kitabia baada ya kuwa na mwenendo mwema.

poza

1. Punguza joto la kitu ili kiwe baridi zaidi. 2. Tuliza aliyekasirika au mpe faraja mwenye huzuni. 3. Malipo ya kumridhisha mtu aliyekosewa.

pozi

1. Mkao wa mwili unaowekwa wakati wa kupigwa picha. 2. Maringo au mbwembwe za kujionyesha.

presha

1. Shinikizo la damu; pia jina la kawaida la hali ya shinikizo la damu kuwa juu. 2. Shinikizo au usumbufu unaomnyima mtu utulivu.

programu

1. Mpango unaoweka utaratibu wa kutekeleza jambo. 2. Mfuatano wa maagizo unaowezesha kompyuta kutekeleza kazi.

protini

Virutubisho vinavyosaidia kujenga na kukarabati mwili, vipatikanavyo katika vyakula vya wanyama na mimea.

pu!

1. Tamko la kuiga au kusisitiza sauti ya kuanguka. 2. Tamko la kuonyesha kukerwa au kuchukizwa.

pua

1. Paka mafuta kwenye mwili. 2. Tumia au maliza kitu chote bila kusaza. 3. Kiungo cha kunusia na kupitishia hewa chenye matundu mawili usoni. 4....

pujua

1. Ondoa ngozi au sehemu ya juu kwa kukwaruza. 2. Punguza uzuri au ubora wa kitu.

puku

1. Panya mkubwa anayejulikana pia kama buku. 2. Kifaa cha kompyuta cha kuhamisha kishale kwenye skrini; kipanya.

pukusa

1. Tikisa mti ili matunda, majani au maua yaanguke. 2. Toboa nafaka au ubao na kuacha ungaunga.

puliza

1. Sukuma hewa kwa nguvu kwa mdomo au pampu. 2. Nyunyiza dawa kupitia bomba la kuipulizia. 3. Legeza uzi wa uvuvi ili samaki akwamuke kwenye ndoana.

puma

1. Hema kwa kutoa pumzi kwa kasi na nguvu. 2. Toa maumivu makali ya ndani, hasa kwa jipu au uvimbe.

pumba

1. Maganda na mabaki yanayotenganishwa na nafaka inapokobolewa. 2. Uchafu unaokusanyika chini ya govi. 3. Mabaki madogo ya nafaka yanayobaki mdom...

pumbaa

1. Kuwa katika hali ya kutoelewa au kufikiri kwa upumbavu. 2. Shikwa na mshangao hadi udumae.