Vinjari kwa Silabi

Silabi: zi

Vimepatikana vidahizo 530 vinavyoishia kwa silabi zi.

Ukurasa 5 / 11 Jumla 530

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

mchunguzi

1. Mtu anayepekua mambo ya wengine yasiyomhusu. 2. Mtu anayefuatilia jambo ili kujua ukweli. 3. Mtu anayefanya utafiti wa kitaaluma.

mkimbizi

1. Mtu mwenye tabia ya kuondoka anapotakiwa kubaki. 2. Mtu aliyeikimbia nchi yake kutafuta usalama kutokana na vita au mateso.

mkombozi

1. Kiongozi wa mapambano ya watu kupata uhuru. 2. Mtu anayelipa ili aliyeshikwa au kilichowekwa rehani kiachiliwe.

mkumbizi

1. Mtu anayekusanya mabaki ya mazao shambani baada ya mavuno. 2. Mtu anayeondoa taka na kuacha mahali safi.

mkwepuzi

1. Mtu anayechukua vitu vya wengine bila ruhusa wala kuvirejesha. 2. Mtu anayekopa kitu na kukataa kukirejesha.

mlanguzi

1. Mtu anayehodhi bidhaa ili aziuze kwa bei ya juu sana. 2. Mtu anayenunua kwa bei ndogo na kuuza ghali ili kupata faida. 3. Mtu anayefanya biash...

mlezi

1. Mfanyakazi anayemtunza mtoto wazazi wanapokuwa kazini. 2. Mtu anayekuza mtoto asiye wake na kumtimizia mahitaji. 3. Uvimbe wa tezi katika sehe...

mlozi

1. Mti unaozaa lozi zenye mbegu ndani ya kokwa. 2. Mwanamume ambaye wake zenu ni ndugu wa familia moja.

mnazi

1. Mti mrefu wa nazi wenye majani kileleni na usio na matawi. 2. Pombe inayopatikana kwa kugema mnazi.