Vinjari kwa Silabi

Silabi: zi

Vimepatikana vidahizo 530 vinavyoishia kwa silabi zi.

Ukurasa 4 / 11 Jumla 530

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

majazi

1. Jina linalolingana na sifa au umbile la mwenyewe. 2. Rehema zinazotoka kwa Mungu.

mapinduzi

1. Kuondolewa kwa watawala madarakani, mara nyingi kwa nguvu. 2. Mabadiliko makubwa ya namna kazi inavyofanywa.

mapokezi

1. Shughuli za kuwapokea na kuwaelekeza wageni. 2. Ofisi ya kwanza ya kupokea wageni katika taasisi.

mashambulizi

1. Vitendo vya kushambulia kwa silaha au ngumi. 2. Majaribio ya timu kupenya eneo la mpinzani na kufunga bao.

mazoezi

1. Matendo ya kuandaa uwezo wa mwili au ujuzi. 2. Kazi za kujifunzia zinazotolewa baada ya somo.

mbukuzi

1. Mtu anayependa kusoma vitabu vingi. 2. Mtu anayepekua na kufichua siri za wengine.

mbuzi

1. Mnyama wa kufugwa mwenye umbo linalofanana na swala. 2. Kifaa cha mbao chenye chuma cha menomeno cha kukunia nazi.

mchafuzi

1. Mtu anayezua fujo au kuharibu uelewano. 2. Mtu anayeharibu mpango wa vitu au shughuli.