Vinjari kwa Silabi

Silabi: sho

Vimepatikana vidahizo 106 vinavyoishia kwa silabi sho.

Ukurasa 1 / 3 Jumla 106

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

aminisho

1. Tendo la kukabidhi mtu au kitu chini ya dhamana ya mwingine. 2. Dhihirisho la nia na utayari wa kutekeleza jambo.

badilisho

Tendo la kugeuza kitu au jambo kutoka hali yake ya awali na kulipa hali, umbo au sura nyingine.

bisho

1. Tendo au sauti ya kugonga mlango ili kufunguliwa. 2. Mwendo au mwelekeo wa chombo kufuata upepo unakoelekea.

fundisho

1. Somo au maarifa anayopatiwa anayejifunza. 2. Onyo linalotokana na jambo baya lililompata mtu.

fusho

1. Kiasi cha baruti kinachoshindiliwa kwenye bunduki. 2. Dawa inayotumiwa katika kufukiza. 3. Ubani au udi unaochomwa katika desturi za tiba.

hasho

1. Kipande cha kuziba ufa au tundu la chombo cha baharini. 2. Kipande cha mti au tambara cha kufunika tundu.

hawilisho

1. Kitu ambacho kimehamishwa mahali kilipokuwa. 2. Tendo la kupeleka mtu au kitu mahali pengine.

jasho

1. Majimaji yanayotoka ngozi ya mwili katika joto au juhudi. 2. Joto la hewa linalomfanya mtu ahisi fukuto. 3. Mapato yanayopatikana kwa juhudi z...

jumlisho

1. Kiasi kinachopatikana vitu vikikusanywa pamoja. 2. Jibu la tendo la kujumlisha namba.

kikausho

1. Kitambaa au sponji ya kuondolea majimaji. 2. Karatasi inayonyonya wino ili maandishi yakauke.

mafundisho

1. Maarifa yanayopatikana kwa kuelekezwa au kufundishwa. 2. Maonyo na ushauri wa kuishi vizuri na wengine.

mchemsho

1. Chakula kinachopikwa kwa kuchemshwa. 2. Mlo wa nyama na vyakula vingine vilivyochemshwa pamoja.