Vinjari kwa Silabi

Silabi: lia

Vimepatikana vidahizo 52 vinavyoishia kwa silabi lia.

Ukurasa 1 / 2 Jumla 52

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

angalia

1. Kuelekeza macho kwenye kitu kwa lengo la kukiona. 2. Kuwa makini na kufanya tahadhari dhidi ya jambo linaloweza kuleta madhara. 3. Kumtunza au...

chalia

Mahali pa kujitenga au kupumzika mwanamke baada ya kujifungua kwa kipindi cha jadi cha siku arobaini.

chukulia

1. Beba kitu kwa ajili ya mtu. 2. Stahimili au zingatia hali ya mtu au jambo. 3. Mweke mtu au jambo katika thamani au mtazamo fulani.

chungulia

1. Angalia kwa siri bila kuonekana. 2. Tazama kupitia tundu au dirisha. 3. Angalia maandishi ya mwingine bila ruhusa.

dalia

1. Poda ya manjano yenye manukato ya kunyunyizia nguo. 2. Unga wenye manukato unaonyunyizwa kwenye sanda.

kimbilia

1. Mfuate mtu kwa mbio ili umfike. 2. Nenda mahali pengine kutafuta usalama au hali bora.

kizalia

1. Sifa au hali inayorithiwa kutoka kwa wazazi. 2. Alama ya mwilini ambayo mtu anazaliwa nayo.

palia

1. Kwamiwa na chakula au maji katika njia ya hewa. 2. Ng'oa au lima magugu kati ya mazao.

shambulia

1. Mwelekee mtu kwa mapigo ya mwili au silaha. 2. Msemeshe mtu kwa maneno makali ya kumuumiza.