Vinjari kwa Silabi

Silabi: ki

Vimepatikana vidahizo 208 vinavyoishia kwa silabi ki.

Ukurasa 2 / 5 Jumla 208

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

hoki

1. Mchezo wa mpira unaochezwa kwa magongo maalumu. 2. Fimbo inayoshikwa na kiongozi wa ngoma au bendi.

itifaki

1. Makubaliano ya pande mbili kuhusu jambo. 2. Taratibu rasmi za kushughulikia shughuli za viongozi.

jeki

1. Kifaa cha kupandishia mzigo mzito. 2. Msaada unaomwezesha mtu kufanya jambo.

kasiki

1. Mtungi mkubwa wa udongo wa kuwekwa wima. 2. Joho la kidini linalovaliwa na kasisi.

kisaki

1. Kwa uimara na nguvu za kutosha. 2. Kiumbe ambacho mfumo wake wa jeni umebadilishwa kwa ufundi wa kijenetiki.

kliniki

1. Kitengo cha huduma kwa wajawazito na wenye watoto wachanga. 2. Kitengo cha hospitali cha kuhudumia maradhi ya aina maalumu.

koki

1. Weka utaratibu wa bunduki katika hali ya kuwa tayari kufyatua. 2. Kifaa cha kufungua au kufunga mtiririko wa maji katika bomba.

laki

1. Enda kumkaribisha mtu anayefika. 2. Idadi inayolingana na elfu mia moja.

maliki

1. Mfalme au mtawala wa kiume. 2. Ubao wa mwanzo unaotumiwa katika kujenga chombo cha majini.

mamluki

1. Askari au mtu anayekodiwa kutekeleza kazi kwa malipo. 2. Mtumwa anayeshiriki vita kama kazi aliyopewa.

metriki

1. Inayohusiana na meta au vipimo vya meta. 2. Mfumo wa desimali wa vipimo unaohusishwa na meta.

miliki

1. Mali iliyo chini ya umiliki wa mtu au shirika. 2. Eneo lililo chini ya mamlaka ya mtawala. 3. Kuwa mwenye mali au kitu fulani.