Vinjari kwa Silabi

Silabi: ka

Vimepatikana vidahizo 600 vinavyoishia kwa silabi ka.

Ukurasa 3 / 12 Jumla 600

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

elekea

1. Angalia au geukia upande wa kitu. 2. Safiri au nenda upande wa mahali fulani. 3. Onyesha dalili kwamba jambo linaweza kuwa kweli au kutokea.

ezeka

1. Funika sehemu ya juu ya nyumba kwa vifaa vya paa. 2. Piga mtu kwa makofi au ngumi.

fafaruka

1. Anguka na kurusha miguu huku na huko bila utaratibu. 2. Sema mengi yasiyokuwa na maana.

faka

1. Utulivu wa moyo au hali ya kustarehe. 2. Nafasi inayomwezesha mtu kutekeleza jambo. 3. Uwezo wa kugharamia au kufanikisha jambo.

falka

1. Sehemu ya ndani ya chombo cha majini ya kuhifadhi shehena. 2. Mlango wa kuingilia behewa la shehena. 3. Vipande vya kitambaa vilivyounganishwa...

faraka

1. Kifaa cha kufumia nyuzi kuwa kitambaa. 2. Hali ya kugawanyika au kutengana. 3. Kipande au sehemu ya kitu.

fika

1. Wasili mahali ulipokuwa ukienda. 2. Timia au wadia kwa wakati unaotajwa. 3. Bila shaka, kwa namna yoyote ile.

foka

1. Chemka ukitoa mapovu hadi kufurika. 2. Toka kwa nguvu kama maji ya chemchemi. 3. Sema kwa ukali na hasira.

fuka

1. Toa moshi kutoka mahali au kitu. 2. Uji mwepesi wa mchele unaotolewa katika desturi kwa mama aliyejifungua.

fumuka

1. Achana kwa nyuzi za kilichofumwa au kushonwa. 2. Achana kwa nywele zilizokuwa zimesukwa.

fundika

1. Suka nywele ziwe na mafundo. 2. Fanya kamba au kitu kingine kiwe na mafundo. 3. Unganisha maua kwa kuyafunga katika uzi.