Vinjari kwa Silabi

Silabi: wa

Vimepatikana vidahizo 176 vinavyoishia kwa silabi wa.

Ukurasa 2 / 4 Jumla 176

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

kolwa

1. Choka na jambo kutokana na kulirudia mno. 2. Pata faida au hali nzuri kutokana na jambo.

lewa

1. Patwa na athari zinazobadili utambuzi kwa pombe au dawa. 2. Shindwa kujimudu kwa kutikisika kwa chombo baharini.

lewalewa

1. Yumba hewani bila kugusa sehemu ya chini. 2. Yumba unapojaribu kusimama au kutembea ukiwa umelewa.

liwa

1. Rojo yenye harufu inayotokana na miti ya mliwa na sandali. 2. Miti inayopandwa kuonesha mpaka wa shamba. 3. Mabua ya mtama ya kutengenezea mit...

maziwa

1. Kimiminika cha titi au kiwele cha mnyama jike. 2. Ute mweupe unaotolewa na mimea fulani.

mheshimiwa

1. Mtu maarufu anayestahiwa sana na watu. 2. Neno la heshima linalotangulia jina au cheo cha mtu.

mkiwa

1. Aliyefiwa na wazazi wote au asiye na jamaa wa kumtegemea. 2. Mtu aliye katika upweke.

mnywanywa

1. Mtu anayeona kinyaa katika karibu kila kitu. 2. Mtu asiyeridhika na kuthamini mambo ya wengine. 3. Mtu mwenye tabia ya kuchagua chakula.