Vinjari kwa Silabi

Silabi: o

Vimepatikana vidahizo 142 vinavyoishia kwa silabi o.

Ukurasa 3 / 3 Jumla 142

Vidahizo

42 kwenye ukurasa huu

pitio

1. Njia nyembamba inayopita kati ya milima. 2. Usomaji wa maandishi kwa makini kwa lengo la kuyachambua.

shikio

1. Sehemu ya kukamatia unapoinua au kutumia chombo. 2. Kifaa cha kuongozea mwelekeo wa chombo cha majini. 3. Kiungo cha kichwani kinachowezesha k...

sukuo

1. Kinoo cha mawe cha kunolea zana za chuma. 2. Msuguo wa kidole katika uso wa anayesutwa.

tao

1. Mkato au pindo la nguo lenye umbo la nusu duara. 2. Umbo la nusu duara katika sehemu ya jengo. 3. Sehemu iliyopinda katika njia au mto. 4. Mw...

ufunguo

1. Kifaa kinachogeuza kufuli ili kufunga au kufungua. 2. Kifaa kidogo cha kurekebisha au kujaza kamani ya saa. 3. Maelezo yanayofafanua alama za ...

ufuo

1. Shimo la kutolea maji wakati wa kuosha maiti. 2. Mfereji mdogo wa maji ya mvua kando ya nyumba. 3. Sehemu ya nchi kavu inayopakana na bahari.

zao

1. Kitu kinachopatikana kwa kuvuna mmea. 2. Mmea unaolimwa kwa lengo la kuvunwa. 3. Jibu la kuzidisha namba.

zio

1. Kipande cha mbao cha kuunganisha sehemu za mtumbwi. 2. Kipande cha mbao cha kuendeshea chombo majini.