Vinjari kwa Silabi

Silabi: ni

Vimepatikana vidahizo 578 vinavyoishia kwa silabi ni.

Ukurasa 6 / 12 Jumla 578

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

majuni

1. Mchanganyiko wenye sukari na dawa za kulevya unaotumiwa kama kileo. 2. Dutu au kitu kinachotumiwa kama dawa.

majununi

1. Mtu anayetajwa kwa dharau kuwa hana akili. 2. Maneno ya kipumbavu yanayoweza kuchekesha.

mani

1. Nyasi zinazoota ardhini. 2. Kipimo cha uzito cha takribani kilogramu moja.

Marekani

1. Kitambaa kigumu cha pamba chenye rangi ya maziwa. 2. Eneo la dunia linalojumuisha Amerika ya Kaskazini na ya Kusini.

maskini

1. Mtu asiye na kipato cha kutosha kujikimu. 2. Mtu mwenye ulemavu anayeshindwa kujikimu na kuomba msaada. 3. Tamko la huruma kwa aliyepatwa na s...

mboni

1. Tundu la katikati ya jicho linalopitisha mwanga. 2. Zawadi inayotolewa kuonyesha mapenzi.

mbuni

1. Mmea unaozaa matunda yenye mbegu za kahawa. 2. Ndege mkubwa asiyeruka mwenye shingo na miguu mirefu.

mdhamini

1. Mtu au taasisi inayosaidia kuendeleza jambo kwa mali au usimamizi. 2. Mtu anayeahidi kutimiza wajibu ikiwa mwingine hatatimiza.

mgeni

1. Mtu asiye wa eneo alilofika. 2. Mtu aliyeombwa kuhudhuria shughuli maalumu.