Vinjari kwa Silabi

Silabi: ka

Vimepatikana vidahizo 600 vinavyoishia kwa silabi ka.

Ukurasa 9 / 12 Jumla 600

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

rika

1. Ngoma nyembamba ya upande mmoja yenye vibati ukingoni. 2. Kundi la watu wenye umri unaolingana au kukaribiana.

ruka

1. Kana ukweli au makubaliano uliyokuwa unayajua. 2. Kuwa fupi mwilini kwa vazi kusinyaa au mvaaji kurefuka.

sadaka

1. Msaada unaotolewa kwa mwenye uhitaji kwa nia ya kupata thawabu. 2. Fedha au vitu vya kusaidia shughuli za ibada. 3. Chakula au kinywaji kinach...

sarifika

1. Kuwa na ufasaha wa lugha unaofuata kanuni. 2. Kuwa na tabia njema inayokubalika. 3. Kuwa katika hali ya kutunzwa vizuri.

shaka

1. Kutokuwa na uhakika kunakoleta wasiwasi. 2. Fukuza mtu au mnyama aondoke.

shalaka

1. Tundu la kamba au chuma linaloshikilia kasia. 2. Kamba inayopitishwa katika roda kwa kutweka tanga.

shereheka

1. Adhimisha jambo kwa shughuli za furaha. 2. Furahi baada ya kushiriki sherehe iliyofanikiwa.

shirika

1. Taasisi au kampuni ya kusimamia shughuli maalumu. 2. Inayomilikiwa kwa pamoja na watu kadhaa.

shoboka

1. Chomoza sana nje, hasa kwa macho. 2. Furahishwa kupita kiasi mpaka hisia zionekane wazi. 3. Konda sana kwa maradhi au maisha magumu.

shughulika

1. Endelea kufuatilia au kutekeleza jambo. 2. Amri ya gwaride ya kujipanga kwa kuangalia upande wa kulia.

shuka

1. Toka sehemu ya juu uende chini au ondoka ndani ya chombo. 2. Pungua kwa kiwango au thamani. 3. Kitambaa cha kutandika juu ya kitanda.