Vinjari kwa Silabi

Silabi: ha

Vimepatikana vidahizo 54 vinavyoishia kwa silabi ha.

Ukurasa 1 / 2 Jumla 54

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

bweha

Mnyama wa porini wa jamii ya mbwa mwenye masikio yaliyosimama na pua ndefu; mbweha.

dhuha

1. Kipindi cha asubuhi baada ya jua kuchomoza na kabla ya adhuhuri. 2. Swala ya suna inayoswaliwa wakati wa dhuha.

fasaha

1. Mwenye kutamka maneno kwa usafi na uwazi. 2. Sahihi na sanifu katika maana au matumizi ya lugha.

furaha

1. Uchangamfu wa moyo wenye bashasha. 2. Hisia ya kuridhika na hali au matokeo. 3. Hali ya kufurahia raha na starehe.

haha

1. Kula kwa pupa na haraka. 2. Vuta na toa pumzi kwa haraka. 3. Ingiwa na hasira na kuhangaishwa na jambo. 4. Babaika katika kauli kwa kuzungumz...

jaha

1. Hadhi ya juu yenye heshima na madaraka. 2. Bahati na neema anayopata mtu. 3. Kwa sauti iliyo wazi kusikika.

kahawa

1. Tunda au mbegu inayotokana na mbuni. 2. Unga wa mbegu za kahawa. 3. Kinywaji kinachotayarishwa kwa unga wa mbuni.

kariha

1. Msukumo unaolazimisha kutenda, hasa unaochochewa na hisia kali. 2. Bahati ya kupata jambo la heri.

madaha

1. Mwendo au tabia ya kujionesha kwa maringo. 2. Mwendo wenye urembo na mpangilio unaopendeza.

mkahawa

1. Mmea unaozaa matunda ya buni za kahawa. 2. Mahali pa kununua chai, kahawa na vyakula vidogovidogo.

mrabaha

1. Malipo ya mwandishi kutokana na mauzo ya kitabu chake. 2. Faida inayopatikana katika biashara. 3. Malipo kwa mwenye mali au rasilimali inayotu...

shabaha

1. Kitu kinachokusudiwa kupigwa kwa mshale, risasi au kifaa kingine. 2. Ustadi wa kupiga kile unacholenga. 3. Jambo ambalo mtu anakusudia kulifikia.

shaha

1. Mtunzi bingwa wa mashairi mwenye daraja la juu sana. 2. Jina la cheo cha mfalme wa zamani wa Iran. 3. Kete ya mfalme katika mchezo wa saratanj...

sheha

1. Kiongozi wa jamii aliyepatikana kwa utaratibu wa mila. 2. Kiongozi wa serikali anayesimamia shehia Zanzibar.