Vinjari kwa Silabi

Silabi: da

Vimepatikana vidahizo 103 vinavyoishia kwa silabi da.

Ukurasa 1 / 3 Jumla 103

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

ada

1. Malipo yanayotolewa ili kupata huduma fulani, kama elimu, burudani au uanachama katika chama. 2. Mila au desturi inayotambuliwa na kufuatwa na ...

akida

1. Kiongozi au kamanda mwenye mamlaka ya kuongoza watu, hasa katika jeshi. 2. Msaidizi wa mkuu wa wilaya katika mfumo wa utawala wa wakati wa ukol...

blenda

Kifaa chenye visu vinavyozungushwa na mota kusaga au kuchanganya vyakula na vinywaji.

buda

1. Mwanaume aliyezeeka. 2. Mtu asiye na meno. 3. Ndovu asiye na pembe, hasa aliyezaliwa bila pembe.

bumunda

1. Kitafunwa cha ndizi mbivu iliyotiwa unga na kupikwa kama andazi. 2. Tonge la duara la unga wa bisi za mtama uliochanganywa na samli.

chonda

1. Hali ya kuwa na huzuni au masikitiko. 2. Hisia ya kutofurahia mafanikio au mali ya mwingine; wivu.

dada

1. Ni mwanamke au msichana mnayeshiriki mzazi mmoja au wazazi wote wawili. Uhusiano huu wa kifamilia unaweza kumhusu aliyezaliwa kabla yako au baad...

doda

1. Baki dukani muda mrefu bila kununuliwa. 2. Jaribu jambo bila kufanikiwa. 3. Kosa kuiva vizuri kwa ugali. 4. Dondoka tone moja moja kwa kimimi...

eda

1. Kipindi cha kusubiri baada ya kufiwa na mume katika Uislamu. 2. Kipindi cha kusubiri baada ya talaka katika Uislamu.

faida

1. Kiasi kinachobaki katika mapato baada ya kutoa gharama. 2. Manufaa yanayopatikana kutokana na jambo.

gida

1. Mimina kimiminika taratibu kutoka chombo kimoja kwenda kingine. 2. Kunywa pombe kwa wingi kupita kiasi.

guda

1. Toa sauti kwa kitu kilichomo ndani kutikisika. 2. Sehemu ya kuegeshea vyombo vya baharini.

jarida

1. Chapisho la mara kwa mara la makala za taaluma fulani. 2. Chapisho lenye makala za mada mbalimbali.

kada

1. Mwanachama anayetetea kwa dhati itikadi ya chama. 2. Mtu wa daraja fulani katika mpangilio wa vyeo.

kasida

1. Tungo za kusifu Mtume Muhammad zinazoimbwa katika Maulidi. 2. Shairi la kuimbwa linalomsifu mtu au jambo.

kiada

1. Ya msingi na iliyotengwa kwa matumizi maalumu. 2. Kwa mpangilio mzuri na utaratibu.