Vinjari kwa Herufi

Herufi: G

Vimepatikana vidahizo 323 vinavyoanza na herufi G.

Ukurasa 1 / 7 Jumla 323

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

-geni

1. Kisichotokana na asili ya mahali kinapotajwa. 2. Kisichojulikana au kisicho cha kawaida.

-gumu

1. Kisicho laini na kisichoharibika kwa kuvunjwa kwa urahisi. 2. Kisicho rahisi kufahamika. 3. Mwenye ujasiri na asiyeogopa. 4. Asiye na huruma....

gadi

1. Mhimili wa mbao au chuma wa kuzuia kitu kisianguke. 2. Zamu ya kutekeleza ulinzi.

gae

1. Kipande kilichovunjika kutoka chombo cha udongo. 2. Mtu mwenye tabia ya kuwachekesha wengine.

gamba

1. Kifuniko kigumu kinachoota juu ya mwili wa samaki au mnyama. 2. Jalada gumu la nje la kitabu.

gambera

1. Msaidizi anayembebea mwindaji bunduki. 2. Mtu anayewaelekeza wenzake namna ya kufanya kazi. 3. Mtu anayetafuta wapenzi kwa niaba ya wengine.

gamti

1. Kitambaa kigumu kisichotiwa rangi, cha namna ya marekani. 2. Aina fulani ya mchele.

ganda

1. Tabaka la nje linalofunika tunda, yai au hindi. 2. Nyumba tupu inayobaki katika risasi. 3. Kuwa kigumu kwa baridi au kugeuka barafu. 4. Zidi ...

gando

1. Sehemu ya kukamata ya kaa au mnyama wa jamii ya chago. 2. Mguu wa kamba, chago au kaa.

gango

1. Tendo au hali ya kufanyiwa tiba. 2. Kifaa cha seremala cha kushikilia vitu vibanane. 3. Sehemu au tendo la kuunganisha vitu. 4. Nyenzo ya kuj...