Vinjari kwa Silabi

Silabi: nya

Vimepatikana vidahizo 91 vinavyoishia kwa silabi nya.

Ukurasa 1 / 2 Jumla 91

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

bambanya

1. Kukarabati kitu kilichoharibika ili kiweze kutumiwa tena. 2. Kufanya kazi bila ujuzi wa kutosha au kwa kubahatisha.

chanya

1. Yenye matumaini mema. 2. Yenye manufaa au inayosisitiza upande mzuri wa jambo. 3. Inayohusishwa na upande wa kuongeza au na thamani kubwa kuli...

fanya

1. Tekeleza kitendo au shughuli. 2. Tengeneza au sanidi kitu. 3. Sababisha hali au jambo kutokea. 4. Chukulia au dhania kuwa hali fulani ipo. 5...

finya

1. Bana kitu kwa ncha za vidole. 2. Kaza sura kwa kuleta mikunjo usoni. 3. Bana kitu kwa kukikandamiza.

gawanya

1. Panga watu au vitu katika mafungu tofauti. 2. Fanya hesabu ya kutafuta mafungu sawa.

jidanganya

1. Jipe matumaini ya kufaulu yasiyo na msingi. 2. Jitwike sifa usizostahili zinazoweza kukudhuru.

jifanya

1. Jionyeshe kuwa na nafasi au hali isiyo ya kweli. 2. Jiweke katika hadhi au hali usiyoistahili.

kandirinya

1. Birika la kuchemshia maji au chai. 2. Birika la fedha au shaba la kunawisha mikono. 3. Muhogo mchungu unaokaushwa kutengeneza makopa.

mwanya

1. Nafasi iliyo kati ya meno mawili ya mbele. 2. Nafasi nyembamba inayotenganisha vitu viwili. 3. Muda mfupi unaopatikana wa kufanya jambo.