Vinjari kwa Silabi

Silabi: no

Vimepatikana vidahizo 149 vinavyoishia kwa silabi no.

Ukurasa 1 / 3 Jumla 149

Vidahizo

50 kwenye ukurasa huu

bano

Kifaa cha kushikilia na kubana mbao, chuma au kitu kingine wakati wa kazi.

chamkano

1. Hali ya kusambaa au kutawanyika. 2. Kikundi cha watu waliotawanyika katika sehemu tofauti. 3. Hali ya kufarakana au kugawanyika kwa watu.

changamano

1. Hali ya kuchanganyika kwa vitu au watu. 2. Hali ya kuelewana, kuafikiana na kufanya kazi pamoja.

kano

1. Nyuzi imara za mwili zinazofunga misuli kwenye mifupa. 2. Msimamo wa kukataa misingi ya dini na maadili.

kifano

1. Mfano wenye ufanano mkubwa na kitu kingine. 2. Muundo wa wastani wa kuwakilisha kitu.

kikono

1. Kamba ya kuunganisha mlingoti na ubavu wa chombo cha majini. 2. Mtu mwenye ulemavu au upungufu wa mkono.

kiuno

1. Eneo la katikati ya mwili kati ya mbavu za chini na makalio. 2. Muundo wa chini wa jengo unaoshikilia ujenzi ulio juu yake.

konokono

1. Kiumbe mwenye mwili laini wenye unyevunyevu na gamba la mviringo. 2. Tunda linalofanana na tomoko.

manjano

1. Rangi inayofanana na ganda la limau lililoiva. 2. Sehemu ya chini ya mmea inayosagwa kuwa kiungo cha njano.