Vinjari kwa Silabi

Silabi: go

Vimepatikana vidahizo 99 vinavyoishia kwa silabi go.

Ukurasa 2 / 2 Jumla 99

Vidahizo

49 kwenye ukurasa huu

mpango

1. Mkakati au utaratibu wa kutekeleza jambo. 2. Namna vitu vilivyowekwa kwa utaratibu.

mtego

1. Kifaa cha kukamatia mnyama, ndege au samaki. 2. Tendo la kutayarisha hali au kifaa cha kunasia. 3. Mbinu anayotumia mtu ili kupata anachokitaka.

mtitigo

Mtikisiko wa chombo kutokana na mawimbi, mashimo ya barabara au hewa yenye misukosuko.

muhogo

1. Mmea wa mizizi yenye wanga na majani yanayotayarishwa kuwa kisamvu. 2. Mzizi uliokomaa wa mmea wa muhogo unaotayarishwa kwa chakula.

mwago

1. Zawadi ya mume kwa mkewe anapotaka kuoa mke mwingine. 2. Sherehe ya kumuaga anayesafiri kwa muda mrefu au anayeolewa.

mwango

1. Nafasi iliyoachwa ukutani ya kupitishia vitu au watu. 2. Mti wenye maua meupe yenye harufu nzuri na magome yanayotumiwa jadi kama dawa au kikol...

mwigo

1. Kufuatisha namna jambo lilivyofanywa na mwingine. 2. Aina ya njiwa anayeaminika kubashiri yatakayotokea safarini.

mwogo

1. Tendo la kuosha mwili ili kuondoa uchafu. 2. Siku iliyotengwa kuwaosha wari wa kumbini pamoja na kungwi wao.

mzigo

1. Kitu kizito kinachochukuliwa, mara nyingi kwa kubebwa kichwani. 2. Mtu anayeonekana kuwa taabu kwa wanaomtegemeza. 3. Jambo gumu linalomsumbua...

ngogo

Samaki mwembamba wa baharini mwenye kichwa kikubwa, masharubu na miiba yenye sumu.

nyago

1. Sehemu ya mguu kutoka nyongani hadi gotini. 2. Hatua inayopigwa wakati wa kutembea.

pango

1. Malipo ya kutumia nyumba au chumba cha mwingine. 2. Tundu kubwa katika ardhi, jabali au mti.

pengo

1. Nafasi iliyoachwa na jino lililotoka. 2. Upungufu unaobaki baada ya mtu muhimu kuondoka.

pigo

1. Kitendo kimoja cha kugonga kwa nguvu. 2. Mkasa unaoleta madhara au huzuni.

pingo

1. Pambo la mpingo linalovaliwa kwenye ndewe. 2. Kipande cha mti cha kukinga mlango kwa ndani.

rago

1. Makazi ya muda ya watu walio safarini au waliohamishwa. 2. Kitu cha kutandikwa kwa kukalia au kulalia.

tego

1. Maradhi ya sehemu za siri yanayohusishwa na uzinzi katika imani fulani. 2. Uganga unaoaminiwa kumnasa anayefanya uzinzi. 3. Zindiko linalowekw...

ubango

1. Nyasi zenye umbo linalofanana na matete. 2. Ganda la tunda la popoo. 3. Msalaba wa Mtakatifu Andrea.

uchaguo

1. Uoneshaji wa unachopendelea kati ya vilivyopo. 2. Uteuzi wa mtu au kitu chenye sifa zinazofaa. 3. Upigaji kura wa kupata wanaotakiwa.

udogo

1. Hali ya kuwa na umbo, umri au cheo kidogo. 2. Hali ya kuwa na vitu au watu wachache.

unyago

1. Mafunzo ya kimila katika kambi ya vijana. 2. Nyimbo na ngoma za mafunzo ya wari.

vugo

1. Ngoma ya wanawake ya pwani inayotumia pembe. 2. Pembe inayotumiwa katika ngoma ya vugo.

zigo

1. Mzigo mkubwa au wenye uzito mwingi. 2. Tatizo kubwa linalomlemea mhusika.