geuza

0

1. Fanya kitu kielekee upande tofauti.

Kitenzi
Mfano wa matumizi Dereva aligeuza gari karibu na Morogoro.

2. Toa upande wa ndani wa kitu uwe nje.

Kitenzi
Mfano wa matumizi Geuza soksi kabla ya kuzifua.

3. Badili kitu kipate umbo, sura au hali mpya.

Kitenzi
Mfano wa matumizi Waligeuza ghala kuwa maktaba.
JIFUNZE ZAIDI

Kuwa Mwanagenzi Mahiri

Fungua huduma zaidi za kukusaidia kuelewa na kufurahia Kiswahili.

  • Maana na utafiti wa kina
  • Picha za vidahizo zinapopatikana
  • Methali zinazotaja neno
  • Viungo vya maneno ndani ya maana
  • Chemshabongo bila kikomo na Vinara
  • Mandhari ya usiku na ukubwa wa maandishi
Fahamu Mwanagenzi Mahiri →