nyoka

Mnyama mrefu, mwenye umbo la mrija, asiye na miguu, hutambaa ardhini, na baadhi ya spishi zake huwa na sumu.

Mnyama wa jamii ya reptilia asiye na miguu na hutambaa ardhini.

Maana

2 jumla

Visawe

1 jumla
fira

Methali zinazotaja neno hili

7 jumla
  • Aliyeumwa Na Nyoka Akiona Jani Hushtuka
  • Fimbo Ya Mbali Haiuwi Nyoka
  • Maneno Mema Hutoa Nyoka Pangoni
  • Mtafunwa Na Nyoka Akiona Unyasi Hushtuka
  • Mtoto Wa Nyoka Ni Nyoka
  • Mwana Wa Nyoka Ni Nyoka
  • Ukitaja Nyoka, Shika Fimbo Mkononi

Asili ya neno

Kiswahili