mzee

0

1. Mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka hamsini hivi.

Nomino
Mfano wa matumizi Mzee alisimulia maisha yake ya ujana mjini Lira.

2. Mtu mwenye nafasi kubwa kazini au mwenye utajiri.

Nomino
Mfano wa matumizi Wafanyakazi walimsubiri mzee wa kampuni awasili.

3. Mzazi wa kiume; baba.

Nomino
Mfano wa matumizi Mzee wangu alinizuru nilipokuwa Moshi.

4. Jina la kumwita mwanamume mwenye wadhifa au mali.

Nomino
Mfano wa matumizi Mzee, tunaomba utupe maelekezo yako.
JIFUNZE ZAIDI

Kuwa Mwanagenzi Mahiri

Fungua huduma zaidi za kukusaidia kuelewa na kufurahia Kiswahili.

  • Maana na utafiti wa kina
  • Picha za vidahizo zinapopatikana
  • Methali zinazotaja neno
  • Viungo vya maneno ndani ya maana
  • Chemshabongo bila kikomo na Vinara
  • Mandhari ya usiku na ukubwa wa maandishi
Fahamu Mwanagenzi Mahiri →