mwiko

0

1. Kifaa chenye mpini mwembamba na ncha bapa cha kusongea au kupakulia chakula.

Nomino
Mfano wa matumizi Mama alitumia mwiko kusonga ugali.

2. Katazo la kufanya jambo kwa kuhofia madhara yanayohusishwa nalo.

Nomino
Mfano wa matumizi Katika mila hiyo, kula chakula kile kulikuwa mwiko.

3. Jambo ambalo mtu hujiepusha nalo kwa imani, msimamo au mazoea yake.

Nomino
Mfano wa matumizi Kwangu mimi, kudanganya rafiki ni mwiko.

4. Kibati chenye mpini kinachotumiwa na mwashi kuchotea na kupaka udongo au lipu.

Nomino
Mfano wa matumizi Mwashi alichota lipu kwa mwiko.
JIFUNZE ZAIDI

Kuwa Mwanagenzi Mahiri

Fungua huduma zaidi za kukusaidia kuelewa na kufurahia Kiswahili.

  • Maana na utafiti wa kina
  • Picha za vidahizo zinapopatikana
  • Methali zinazotaja neno
  • Viungo vya maneno ndani ya maana
  • Chemshabongo bila kikomo na Vinara
  • Mandhari ya usiku na ukubwa wa maandishi
Fahamu Mwanagenzi Mahiri →