bari

0

1. Kuweka chombo kando au mbali na vingine ili visigongane.

Kitenzi
Mfano wa matumizi Kasongo alibari chupa na vyombo vingine ili isipasuke wakati wa safari.

2. Kukaa kando au kujitenga mbali na kitu.

Kitenzi
Mfano wa matumizi Mtoto alijibari na jiko lililokuwa na moto.

3. Kujinyima au kuacha kufanya jambo kwa sababu maalumu.

Kitenzi
Mfano wa matumizi Alijibari na starehe ili akamilishe masomo yake.

4. Jina au sifa ya Mungu inayomhusisha na kuumba viumbe.

Nomino
Mfano wa matumizi Katika dua, alimtaja Mungu kwa jina Bari.
JIFUNZE ZAIDI

Kuwa Mwanagenzi Mahiri

Fungua huduma zaidi za kukusaidia kuelewa na kufurahia Kiswahili.

  • Maana na utafiti wa kina
  • Picha za vidahizo zinapopatikana
  • Methali zinazotaja neno
  • Viungo vya maneno ndani ya maana
  • Chemshabongo bila kikomo na Vinara
  • Mandhari ya usiku na ukubwa wa maandishi
Fahamu Mwanagenzi Mahiri →